Saturday 4 January 2014

MSANII DAYNA NYANGE ATOA YA MOYONI JUU YA WATU WALIVYOPOKEA TAARIFA YA KUSHIKWA KWA VIDEO QUEEN JACK CLIFF

MSANII WA KIZAZI KIPYA DAYNA NYANGE
Jamani hivi ni nani kwenye Mgongo huu wa dunia ambaye hajawai kukosea?!
Wapo binadamu wenzetu wanamakosa makubwa na hatuyajui na mengine yanajulikana....
Kwanini tumekuwa mstari wa mbele kuwanyooshea watu vidole pale wanapokosea tena na kuwaombea Mabaya....... Dah!
Tukumbuke Sisi sote ni binadamu akuna anaejua kesho yake
Sina maana tutetee uovu au kosa linapofanyika bali tutumie muda kutafakari kabla ya kumhukumu MTU..
Wanawake wenzangu huyu ni Mwanamke mwenzetu lakini sisi ndio tumekuwa mstari wa mbele kumlaani Na kutolea maneno machafu Na hali Yakuwa tunajua hakuna alie mkamilifu
Binafsi imeniuma Na nimejiskia vibaya sana

SAWA KAFANYA KOSA
Ila tusiwe majaji wa kutoa hukumu anza kujihukumu kwa maovu yako kabla ya kumuhukumu mwenzako
Tafakari maovu yako kabla kumnyooshea kidole mwenzako

Tuache mamlaka za sheria zifanye kazi yake
Wanawake wenzangu TUPENDANE Na tuwe na umoja Tushirikiane na tushauriane katika maamuzi yetu madogo Na makubwa labda tutaepuka ili tatizo
Inawezekana haya yote yanatokea kwetu sisi kwa kukosa ushirikiano Na upendo

JACK DADA ANGU UMEKOSEA
Ila Sina sababu ya kukulaumu au kukuhukumu
wakati mwingine binaadamu ujifunza katokana Na makosa Mungu ni wetu sote Inshaallah atakusimamia katika hili.
Nimeshidwa kuvumilia nimeamua kusema nilichosema ila kama Kuna nilie mkwaza
naomba Aniwie radhi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA
By Dayna nyange

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako