Wednesday 1 January 2014

DIAMOND ALIVYOFUNGA MWAKA NDANI YA LINDI

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayetikisa Nchi ya Tanzania na Africa kwa Ujumla, Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond, ameuanza mwaka mpya na wananchi wa Lindi katika tamasha la kudumisha Amani na maendeleo lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Bernard Membe.
Tamasha hilo limefanyika usiku wa kuamkia mwaka 2014 katika uwanja wa Ilulu Manispaa ya Lindi ambapo Diamond amezikonga vyema vyoyo za wananchi wa Mkoa huo.
 
Mbunge aliyemwalika Diamond ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe, Bernard Membe naye alikuwepo sambamba na wananchi wa Lindi kushuhudia shoo hiyo iliyoambatana na kuukaribisha mwaka 2014

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako