Wednesday 1 January 2014

MWANAHIP-HOP WA MAREKANI AANDIKA POST YENYE NENO LA KISWAHILI

 
Mwaka mpya wa 2014 tunauanza vizuri kabisa watanzania baada ya siku moja kabla ya kuumaliza mwaka huo wa 2013 msanii wa Marekani wa mtindo wa kufoka foka ameandika status kyenye neno la Kiswahili kwenye Account yake.
Talib Kweli (38), aliweka neno la Kiswahili kwenye moja ya sentensi zake ndani ya mtandao wa twitter alio na wafuasi zaidi ya laki nane huku akiwa anafwatwa na mastaa kadhaa wa bongo akiwemo Nikki wa II, Godzilla, Profesa Jay, Chidi Benz, Fid Q, Vanessa Mdee na wengine.
Wakati kilipotokea kifo cha mzee Nelson Mandela, staa wa hiphop duniani Nicki Minaj alimiliki headlines kwenye nchi zinazoongea Kiswahili baada ya kuandika ujumbe kuhusu mzee Mandela na kisha kumalizia kwa kuandika kiswahili ‘madaraka kwa wote’ kwenye page yake ya Instagram.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako