Sunday 5 January 2014

MUDADA AJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MPIGO


Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, amejifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya. 
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Watoto hao mapacha wana uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi na wapo katika hali nzuri 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako