Friday 17 January 2014

PROF. JAY KUMSHIRIKISHA DIAMOND NGOMA MPYA


Muasisi wa Bongo Flava Joseph Haule a.k.a Prof Jay ambae alifanya vizuri na anaendelea kufanya vizuri katika muziki huu wa bongo fleva akiwa na miaka mingi katika muziki huo.
Prof Jay alisema "Nipo kwa producer wangu mkongwe P funk Majan, Tuanaandaa kitu kikubwa kwa ajili ya mashabiki wanaopenda muziki mzuri. Ila  ngoma hii nimemshirikisha Diamond Platnumz, kwani yote hii ni kuleta umoja kati ya wasanii wa zamani na wasasa pia na uwezo wa msanii Diamond."
 

Ngoma hii itakuwa audio na video kwa mara moja, video atafanya mkongwe pia katika tasnia ya hiyo ya video ambae ni Adam Juma. Yote haya ni hivi karibuni maana nipo mwishoni kumaliza vyote ili watu wangu wapate burudani nzuri.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako