Wednesday 8 January 2014

KESI YA JACQULINE PATRICK KUSIKILIZWA 2016


Kesi ya yule Star wa bongo Jacqueline Patrick aliyekamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Macau China, itaanza kusikilizwa Mwaka 2016.
Hiyo ni kutokana na Jack kutojua Lugha ya Kireno ambayo ndio itatumika huko Macau na pia ndio lugha ambayo itatumika katika Hukumu ya kesi hiyo.
Jack alikamatwa na dawa za kulevya, December 19 mwaka jana uwanja wa ndege Macau China akitokea Bangkok Thailand akiwa na kete 57 (kilo1.1) za heroin tumboni zenye thamani ya shilingi milioni 300. 
Jacqueline amepewa mwaka mmoja na nusu (siku447) ajifunze kireno, lugha inayozungumzwa na watu wa Macau ambayo itatumika mahakamani wakati kesi yake ikisikilizwa.
Sheria ya kisiwa hicho inasema kuwa mshtakiwa yeyote atakayepelekwa kortini kesi yake haitasikilizwa mpaka majaji wakubali kuwa anaijua lugha hiyo na siyo kinyume na hapo.
 
Jack amepewa mwalimu maalumu anayejua lugha za kiingereza na kireno, ndiye atakayemfundisha mpaka atakapojua.

1 comment:

Ahsante kwa Maoni yako