Sunday 12 January 2014

MTOTO AJICHOMA MOTO BAADA YA KUKATALIWA KUOA BINTI WA DINI TOFAUTI


Kijana Mansur Tanko (21) mwenye dini ya kiislam amejichoma moto hadi kufa kwa kukataliwa na baba yake kumuoa binti wa kikristo aliyempenda.
Shuhuda wa Tukio hilo Alhaji Jibrin Bala alisema Mansur amejichoma moto hadi kufariki baada ya baba yake Tanko Mijinyawa kukataa ombi la mtoto la kumuoa binti wa dini tofauti (mkristo)
"Monsur alikuja na ombi la kutaka baraka kutoka kwa baba yake juu ya suala la kufunga ndoa na binti wa kikristo anayempenda, ila baada ya kumwambia baba yake akakataa kata kata moto wake kumchumbia binti huyo, baada ya kuona hivyo Mansur akaenda kulia kwenye moja ya kingo za nyumba, mara ghafla tukaona moshi mweusi kwenda kuangalia tukakuta Mansur akiwa anateketea kwa moto"
"baba na watu wengine wakajaribu kuuzima moto huo bila mafanikio, ambapo Mansur alikuwa ameshaungua vibaya na walipomkimbiza Hospital alikuwa ameshafariki kwa majeraha makubwa ya moto"
Msemaji wa kituo cha Polisi Taraba, bwana Joseph Kwaji amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako