Wednesday 29 January 2014

RAIS WA BARCA ATAKA MESSI AONGEZEWE MSHAHARA, AMZIDI RONALDO


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hauzwi na klabu hiyo inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina, amesema rais wa klabu hiyo Joseph Maria Bartomeu.
Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d’Or, mwenye umri wa miaka 26, anatakiwa na matajiri wa klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain.
Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1, yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema: “Klabu itakaa na kuangalia mkataba mpya. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi duniani.”
Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50 aliyocheza msimu uliopita na hadi sasa amefunga mabao 18 na manane kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako