Wednesday 29 January 2014

MSANII WA NIGERIA KCEE, AMLIPA NICK MINAJ MIL. ZAIDI YA 650 KUFANYA NAYE WIMBO


Habari kutoka kwenye mtandao moja wa burudani wa Nigeria zinadai kuwa msanii, KCEE ametoa kitita cha sh. zaidi ya milioni 650 kufanya wimbo na msanii wa kimataifa Nick Minaj.
"Tupo nchini Marekani kujaribu kupata Collaboration, Ni kweli tupo kwenye mchakato wa kufanya wimbo na Nick Minaj. Tulitaka kuifanya iwe ni Suprise kwa mashabiki lakini kwa kuwa tayari imejulikana hatuna budi kusema ukweli huo" Alisema 
Wakati mambo yakitaarifiwa hivyo, Meneja wa msanii huyo aligoma kutaja kiasi cha pesa walizompa Nick Minaj, "Kweli tumempa pase Nick Minaj ili tufanye naye Ngoa ila kiasi ni Siri yake, na kwa taarifa tu tunataka kuongeza msanii mwingine kutoka YMCMB ambaye ni zaidi ya Nick Minaj, Nick Mwenyewe ameshadhibitisha kufanya wimbo na KCEE ila huyo mwingine mtamjua tu" 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako