Sunday 5 January 2014

EUDOXIE AAHIDI KUFUNGA NDOA NA LUDACRIS JAPO AMEZAA NJE


Mpenzi wa muda mrefu wa Ludacris Eudoxie amefunga macho na kujifanya haoni ubaya alioutenda Ludacris kwa kupata mtoto nje ya uhusiano wao, ambapo ameahidi kufunga naye ndoa.
Habari kutoka rafiki wa karibu zinasema kuwa, Eudoxie ameshamsamehe Ludacris kwa kumpa ujauzito mama mtoto wa Luda, Tamika Fuller 
Luda alijitetea ya kuwa tulio hilo lilitokea bahati mbaya wakati wakiwa kwenye hatua za mwisho za kuachana na Tamika
Akimzungumzia Eudoxie, mpashaji habari amesema Luda yuko kwenye uhusiano na Eudoxie tangu 2009, na kiukweli imemuumiza sana kusikia taarifa hizo za mtoto, japo walipata nafasi za kuyaongea na kuyamaliza.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako