Wednesday 1 January 2014

UJUMBE ALIOANZA NAO MWAKA 2014, JOYCE KIRIA KWA WAKINADADA


Hakianan huu ujumbe nauleta kwako kwa nia njema kabisa kwa ajili ya kumaliza 2013.
we Mwanamke mwenzangu ambae mpaka sasa bado unategemea mwanaume akuendeshee maisha kwa kila kitu, hakika unaitaji Ukombozi..
Siyo dhambi kama ukipata mwanaume anaekugaramia kwa vitu mbalimbali kwa hiari yake na mapenzi yake..siyo kwa kudai kama vile umemwajiri au ulimkopesha!!
Tatizo letu wengine tunawalazimisha wapenzi wetu watufanyie vitu kwa nguvu na asipofanya hivyo Utanunaje sasa!! 
Mbaya zaidi Mara nyingi mnaomba vitu ambavyo wapenzi wenu hawana uwezo navyo! Na wewe mwenyewe mwanamke umeshindwa kujiuliza kwamba mbona wewe huna hivyo vitu unavyolazimisha ununuliwe? Yeye akaibe??
Unakuta mtu katongozwa tu! Anaanza oooh kodi imeisha, oooh nadaiwa ada, nataka galax note3, oooh nataka kiwanja, oooh nataka nyumba, oooh nataka gari, vocha, bili ya maji, umeme, nauli ya kwenda kusalimia ndugu na jamaa, oooh simu ya mama, !! Kiruuuuuuuu ndo maana wanaume wenye akili zao wanatoka baru...
Jamani wanaume siyo Migodi! Nao wanatafuta pesa kwa tabu sana.siku hizi maisha ni magumu sana, Ujumbe wangu wa kuanza 2014 Tushirikiane kuleta maendeleo yetu pamoja badala ya kugeuzana ATM...
Huu ujumbe kama umekugusa hakikisha unaingia 2014 ukiwa na mtazamo mpya tofauti na huo wa Kitumwa na epuka kabisa kuwa Mzigo kwa mwenzako....kuwa msaada kwake ili maisha yawe mepesi...
Hata wanaume siku hizi wapo Magolikipa...acheni siyo fresh

Mbutaaaaaa...

NOTE: USISAHAU OPERESHENI TOKOMEZA MICHANGO YA HARUSI NA SHEREHE 2014..Tuchangie maendeleo..

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako