Saturday 21 December 2013

WAVUNJA REKODI KWA KUZUNGUKA NA BAJAJI DUNIA NZIMA


Watanzania wengi tunafahamu Bajaji ni usafiri wa hapa na pale tu, yani sio usafiri wa kubeba abiria kwenye masafa marefu lakini Walimu wawili raia wa Uingereza wamekipiga kibajaji gia na kupita nacho nchi mbalimbali duniani zinazofikia 37.
Ni safari ambayo wameianza August 13 mwaka jana (2012) lakini haijafikia hapa bila matatizo, wanakwambia Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya nchi na kuna wakati injini ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka wakati mwingine wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.
Ndani ya Nchi ya Hispania
Unaambiwa hii rekodi itaingia kwenye kitabu cha Guiness kama watamaliza safari yao ambayo wamepanga kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha kurudi zao nyumbani Uingereza.
Wakiwa na Vijana wapiganaji Nchini Burundi
Wanasema wengine wameshindwa kuamini kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a Bajaji ambapo kwenye mpaka wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi ambae aliwaambia haamini kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli, itakua ngumu wao kupata watoto wa kiume, labda wa kike. 

Ndani ya Nchi ya Ethiopia
Ndani ya Hispania
Wakivinjari katika mnara maarufu Nchini Ufaransa-paris
Wakiwa wamepumzika na Bajaji yao Nchini Afrika Kusini
Wakilamba vumbi Nchini Tanzania
Wakiivuta Bajaji baada ya Kusumbua Huko Msumbuji

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako