Saturday, 21 December 2013

SIMBA ILIVYOIFUNGA YANGA 3-1 TAIFA LEO

Mechi ya Nani Mtani Jembe yakamilika kwa timu ya Simba Sc kushinda magoli 3 ambapo magoli mawili yamefungwa kipindi cha kwanza na goli moja limefungwa kipindi cha pili na kukamilisha magoli 3 kwa timu ya Simba.
Miongoni mwa makosa yaliyoelezwa na wachambuzi wa mechi hii ni kujiamini kwa timu ya Yanga.
Magoli mawili ya Simba yamefungwa na Hamisi Tambwe na  Awadh Juma ametupia goli moja.
Upande wa Yanga lilifungwa na Emmanuel Okwi ambaye ni mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga
Golikipa wa timu ya Yanga Juma Kaseja akiondosha moja ya hatari iliyokuwa inaenda langoni mwa timu yake
Golikipa wa Timu ya SImba, Ivo Mapunda akiurukia mpira juu na kuudaka usilete madhara kwanye lango la timu yake 
Wachezaji wa Timu ya SImba wakishangilia goli lao la kwanza lililopatikana mnamo Dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza 
Mashabiki wa Timu ya Simba wakishangilia Goli kwa nguvu zote
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Mrisho Ngassa akimpiga chenga ya mwili beki wa Timu ya Simba, Donald Mtosi wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe uliomalizika hivi punde ndani ya uwanja wa Taifa 
Mchezaji wa Timu ya Simba, Hamis Tambwe akipiga penati iliyoingia moja kwa moja golini na kuiandikia Simba bao lake la pili katika Dakika ya 42 ya mchezo wa Nani Mtani Jembe uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
Beki wa Timu ya Yanga, Kelvin Yongani (katikati) akiondoka na mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Simba
Mashabiki wa Timu ya SImba wakishangilia kwa Furaha ushindi wa goli 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyoisha muda si mrefu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako