Sunday 15 December 2013

PETE INAYOWEZA KUPOKEA SIMU, REMOT CONTROL NA KUUNGANISHWA NA SMARTPHONE YAGUNDULIWA


Mwezi mitatu toka Kampuni 3 maarufu duniani zitoe Smartwatches na kuziuza sokoni sasa Teknolojia inazidi kuongezeka na kufika mbali.
Engineer Ashok Kumar kutoka Chennai, India amebuni kitu kidogo zaidi ambacho amekiita Smartring, ambayo ni pete ya kuvaa kwenye kidole inatengenezwa na uwezo wa kupokea Bluetooth "Bluetooth 4.0 sensor" inayoweza kuunganisha na simu yeyote ya Android au IOS kupitia application maalum inayopatikana kwenye Smart Ring.
Smart ring inauwezo wa kuunganishwa na aina hizo za simu na kutoa taarifa (notification) pindi ujumbe na barua pepe zinapoingia katika simu, huku mtumiaji akii-control hiyo simu yake kwa kutumia smart Ring hata kama simu iko mbali na yeye.
Smart Ring in a vitufe vinavyoweza kupokea simu na kuplay muziki uliopo kwenye smartphone ya mtumiaji, pia kwenye kioo (Screen) ua pete hiyo huwaka pindi mtu aliyeivaa anapopokea e-mail, sms, faceboo na Twitter notification au simu inapoingia bila kusahau pete hiyo inaweza kutumika kama remote control.
Panapokuwa hakuna notification yeyote pete hiyo huonyesha muda kwenye screen yake na pale simu inapoingia ndipo hubadilika na aliyeivaa ana uwezo wa kuchagua kupokea au kuikata simu iliyoingia kwa kutumia buttons ambazo ziko pembeni mwa pete hiyo.
April, 2014 ndipo rasmi Smart Ring zitaanza kuingia sokoni kuuzwa na bei yake inakadiriwa kuwa Tsh. 442,000/= ($275)
Mwezi wa tisa mwaka huu (September, 2013) wabunifu kutoka Hungary walitambulisha pete ka ahiyo iliyopewa jina la "Ring Clock" ambayo ilikuwa inaonyesha muda peke yake ila huyo jamaa wa India kaongeza maujanja zaidi 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako