Sunday 1 December 2013

PAUL WALKER AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI


Mwigizaji maarufu Duniani “Paul Walker” aliyekuwa mwongozaji wa Movie na thamthilia ya “Fast and the Furious” amefariki Dunia Jumamosi ya Novemba,30 kwenye ajali ya gari katika eneo la Valencia, Calif,
Paul walker amefariki akiwa na umri wa miaka 40, huku wenzake kwenye kampuni yao ya Universal wakishindwa kuamini Taarifa hizo za kifo chake.
“Watu wote hapa studio za Universal tumevunjika mioyo” mwakilishi wa Studio alisema na kuongeza  “Paul alikuwa mwaminifu na mmoja kati ya wasanii wanaopendwa katika studio hizi kwa miaka 14 na kufariki kwake ni pigo kwetu na kwa kila mmoja anayehusika kwa namna yeyote kwenye “Fast and Furious’ films”
“tunatuma salamu zetu za pole kwa familia ya Paul kwa msiba huu mzito”
Akkaunti za mitandao ya Twitter na facebook za Walker zilithibitisha taarifa hizo za kufariki kwa Paul walker baada ya kuripotiwa na mtandao wa TMZ
Salamu za Rambirambi zimeendelea kutumwa kwa wingi saa 1 baada ya kuandikwa kwa uthibitisho huo wa kufariki kwa Paul Walker

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako