Tuesday 31 December 2013

KUAPISHWA KWA IGP NA NAIBU WAKE LEO JIONI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini.
Rais Jakaya mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Jioni
Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu Saidi Mwema.
Rais Jakaya mrisho Kikwete, katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni hii
 Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho Januari Mosi 2014 Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi la Polisi Tanzania.
Rais Jakaya mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu Inspekta Generali wa polisi (IGP) Mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Leo Jioni 
Rais Kikwete alimteua pia Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi na kumuapisha siku ya leo kuchukua nafasi hiyo atakayoanza kuitumikia rasmi kesho nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi nchini.
Rais Jakaya mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na IGP mstaaafu Afande Said Mwema pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo jioni
Kabla ya uteuzi wake Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations)
Rais Jakaya mrisho Kikwete, Makamu wa Raisi Dkt. Mohamed Ghalib Bilali, Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni hii 
Rais Jakaya mrisho Kikwete, Makamu wa Raisi Dkt. Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako