Tuesday 3 December 2013

WASANII WA MUZIKI NA MOVIE ZA KISWAHILI PATRICK BASHIZ NA MAGGIE SELUWA WAFUNGA NDOA NCHINI DENMARK


Wasanii wa movie za kiswahili pamoja na muziki wenye makazi yao nchini norway Patrick Bashizi na Maggie Seluwa wafunga Ndoa.
Wawili hao wamedhihirisha upendo wao wa kweli uliyodumu kwa muda mrefu katika hali ya uchumba na sasa wameamua kuudhihirishia ulimwengu juu ya upendo wao kwakufunga ndoa ya kifahari iliyohudhuriwa na watu maarufu nchini denmark.
Harusi hiyo ya kipekee ilifanyika juzi tarehe 30 mwezi November katika nchi ya denmark walipo wazazi wa Maggie Seluwa, huku wazazi na ndugu wa Patrick wakijumuika kwa pamoja kutokea Norway wanapoishi, Awali akizungumza na blog ya Patapicha mama wa msanii huyo wa movie kutoka Norway alisema anafurahia sana mwanae kuanza maisha mapya.
 “Kiukweli namshukuru mungu sana mwanangu kutimiza adhima yake yakutaka kuowa na sasa kafanikiwa kwakweli mungu ni mwema sana” alisema mama patrick kwa furaha sana.
Kwa upande wa Maggie Seluwa ambaye ana vipaji vingi vinavyomfanya aheshimike nchini Norway amesema hana la kuongea kwa sasa zaidi ya kumshukuru mungu kwa kufanikisha kuwa na mtu anayempenda kwa dhati na ambaye alikuwa akiota kila siku kuja kuishi nae kama mke na mume japo wamekuwa wachumba kwa muda sasa
Kaka namsukuru sana mungu kwa kunipa mume ambaye alikuwa katika maisha yangu siku zote kwa shida na raha kiukweli nampenda sana mume wangu na mungu atupe maisha marefu pia nawashukuru wote walioshiriki kufanikisha harusi yetu kwa namna mmoja au nyingine kwani hatuna cha kuwalipa ila mungu atasema nao kwakila aliyetumia mali au muda wake kutu-support sisi katika harusi yetu” alisema msanii huyo muigizaji, muimbaji na mwanamitindo maarufu nchini Norway.
Wasanii hawa kwa sasa wanampango wakuwekeza Tanzania katika filamu za kimataifa na wamedhamiria kuwaleta mastar wakubwa wa filamu kwa ajili ya kuinua kiwanda cha filamu tanzania.
Akizungumza na mwandishi wa patapicha mapema Patrick amesema.
Kaka nadhani furaha yangu imekamilika sasa sikuwa nasubiri furaha zaidi ya hiyo namshukuru mungu tumemaliza salama na kila kitu kimeenda sawa hivyo kwasasa ahadi yangu ya kuja afrika kwaajili ya kuwekeza katika soko la movie ipo pale pale na soon nitaadha kulishughulikia ili kubadili mfumo wa movie zetu” alisema Patrick ambaye pia ni mchezaji na muongozaji aliyesomea na kupata cheti cha kuongozaji filamu


No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako