Monday 23 December 2013

LORD INFAMOUS WA KUNDI LA THREE SIX MAFIA AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa member wa kundi maarufu la Three Six Mafia, Rapa Ricky Dunigan(40) a.k.a Lord Infamous amefariki Dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa mama yake anayeishi Memphis.
Dj  Paul ambaye ni member wa kundi hilo amedhibitisha kutokea kifo cha Infamous huku akidai sababu ya kifo chake bado hakijafahamika.
Kundi hilo linalofanya muziki wa HipHop linaloundwa na wasanii mahiri kama Dj Paul,  Juicy J,  Lord Infamous, Gangster Boo, Cruchy Black na KoopStar Knicca kutokea Memphis, Tennessee nchini Marekani , lilianza kusikika kuanzia miaka ya1994 huku albamu yao ya Mystic Stylez ikiwatambulisha katika ulimwengu wa muziki.
Hii ni moja ya Tweets aliyotweet memba wa 3 Six Mafia Lola a.k.a Boo baada ya kutokea kifo cha Infamous. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako