Monday 23 December 2013

MOTO WATEKETEZA MADUKA 10 STENDI YA MABASI MSAMVU MOROGORO

MOTO Mkubwa uliowaka  jana usiku zaidi ya masaa manne mfululizo umeteketeza maduka zaidi ya 10 yaliopo eneo la Msamvu Morogoro jirani na stendi kuu ya mabasi ya ya mikoani.
Wakihojiwa na Mtandao huu baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba chanzo cha moto huu ni hitirafu ya umeme iliyotokea kwenye baa ya Terminal Pub na moto huo kusambaa kwenye maduka mengine.
"Baada ya kutokea hali hiyo moto ulishika kasi kubwa na kuwashinda watu wa fanya ambapo ulianza kuwaka saa nane usiku mpaka muda huu saa 12 asubuhi bado unawaka kama unavyouona"alisema Bw Agustino Massawe.
Juhudi za Mtandao huu za kuzungumza na Mmiliki wa jengo hilo lenye maduka zaidi ya 30 mzee Melle ziligonga ukuta baada ya mzee huyo kutoonekana eneo hilo la tukio.
Hadi mtandao huu una kwenda mitambo hakuna mtu yoyote aliyekuwa tayari kuzungumzia hasara zilitopatikana kwenye janga hilo kufutia wamiliki wote wa maduka hayo kuwa bize kuokoa mali zao

 
SOURCE: SHEKIDELE BLOG

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako