Monday 23 December 2013

DIAMOND AENDELEA KUTOA ZAWADI ZA X-MAS KWA WATOTO YATIMA

Diamond amerudi kwao Tandale kwenye kituo cha Al Madina kilichopo Tandale Yemen kuwapa watoto zawadi za Christmas na kupata nao chakula cha mchana.
Wiki iliyopita Diamond alienda kwenye kituo kilichopo Buguruni Malapa na kesho Jumanne ataenda Kigogo kwenye kituo cha New Life.
Baada ya kutoa zawadi za Christmas kule Buguruni alisema kwamba ataendelea kutoa zawadi nyingine kwenye vituo mbalimbali na anawakaribisha watu wengine waungane naye kuwapa watoto zawadi kwenye msimu huu wa sikukuu.
Zawadi hizo zinaambatana na mialiko kwa watoto hao kwenda kwenye show yake maalum kwa ajili ya watoto itakayofanyika siku ya Christmas pale Leaders Club.
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako