JINA
KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A.K.A:
Mandela
MAJINA YA
UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI
ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI:
Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA
KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA
KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI
ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan,
Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha
Witwatersrand, Johannesburg.
Nelson
Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye
alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto
wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji
mdogo wa Transkei.
CHAMA CHA
ANC
Mandela alisoma katika Chuo Kikuu cha Fort Hare na
Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Akawa mwanasheria mwaka 1942. Mwaka 1944,
alijiunga na Chama cha ANC, chama kilichodhamiria kuutokomeza utawala wa
makaburu weupe pekee. Mwaka 1960, Chama tawala cha makaburu kilikipiga marufuku
cha cha ANC na kuwashitaki viongozi wake kwa kosa la uhaini, lakini Mandela
aliachiwa huru.
Rais Barack Obama akiwa ndani ya chumba cha gereza alimokuwa akiishi Mandela akitumikia kifungo chake cha maisha. |
KUFUNGWA
GEREZANI
Akiendeleza harakati zake za kupambana na makaburu,
Mandela alikamatwa, akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani
kuanzia mwaka 1964 hadi 1990, ambapo maisha yake kama kiongozi wa harakati za
kupambana na ubaguzi wa rangi yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa
dhamiri, Mandela mara kwa mara alikataa kuachiwa kwa masharti.
Mandela akiwa ndani ya chumba cha gereza alimokaa kwa miaka 26, hapa alikwenda kutembea baada ya kuwa rais |
KUACHIWA
HURU
Mwaka 1990, akiwa amekaa jela kwa miaka 26 na akiwa
na umri wa miaka 71, iliachiwa huru bila masharti yoyote baada ya utawala wa
kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa. Mwaka 1993, Nelson Mandela
alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake za kisiasa.
MAISHA YA
URAIANI
Mwaka
1994 akiwa katika umri huo, Mandela aligombea kiti cha uraisi na kushinda akiwa
raisi wa kwanza mweusi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako