Monday 16 December 2013

AZAM TV YAZINDULIWA RASMI LEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akikata akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington

AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akisalimiana na baadhi ya waigizaji wa Filamu nchini kutoka kundi la (Bongo Movie) waliokuwepo kwenye Ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar
Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kuangalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akizungumza na vyombo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo kwenye ufunguzi huo wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam
Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akizungumza jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington mara baada ya Ufunguzi wa Jengo la Ofisi za Azam TV jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni hiyo,Mehboob Aladdad
·         Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
·         Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
·         SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington akisisitiza jambo mbele ya waandishu wa habari (hawapo pichani) juu ya huduma mbali mbali wazitoazo kama Azam TV
Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.

“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
Rhys Torrington: 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV  ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. 
Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – sio tu katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako