Friday 13 December 2013

LOWASSA ANUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE


Waziri mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa monduli Mhe. Edward Lowassa amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa amepanda akiwa na abiria kadhaa kupasuka matairi yote manne, leo mchana.
Ndege hiyo ya Shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha.
"yaani Mungu ni Mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Mhe. Lowassa… mungu atamlinda jamani.. sioamini" alisikika akisema mama mmoja aliyekuwemo kwenye ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako