Basi la kwanza la mradi wa
mabasi yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika
barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka
kesho.
Mtendaji mkuu wakala wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa
mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na
makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es
Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha
ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.
Nao baadhi ya wakazi wa jiji
walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na
serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa
utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku
wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi
hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako