Vikosi vya Kenya vimezidi kuongezwa kwenye eneo la
maduka la westgate, Nairobi ambapo watu wanaodhaniwa kuwa ni Al-shabab
wameendelea kulishika jengo hilo na mateka kadhaa.
Hadi sasa watu wapatao 59 wameripotiwa kuuwawa na wengine
175 kujeruhiwa huku kukiwa hakuna idadi maalum ya mateka waliokwama ndani ya
jengo hilo.
Al-shabab wametuma
ujumbe kwenye akaunti yao ya Twittwer wakithibitisha kuhusika na tukio hilo,
huku wakisifia kuwa vijana wao bado wameweza kulishikilia jingo hilo kwa masaa
20 sasa.
Rais wa Kenya,
Uhuru Kenyatta ameomba umoja kwa raia wa nchi hiyo katika kipindi hiki kigumu
na kusisitiza kuwa wahusika wa tukio hilo watakamatwa popote walipo iwe ni
ndani ya nchi ama nje ya nchi hiyo.
Tayari nchi kadhaa
zimethibitisha kupoteza raia wao katika tukio hilo.
Rais wa Ufaransa
Francois Hollande ameliita shambulizi hilo ni la kiwoga. Imeripotiwa kuwa raia
wawili wa ufaransa ni miongoni mwa waliokufa.
Wakati Marekani
ikidai kuwa ina raia wake kadhaa waliojeruhiwa katika tukio hilo, Kanada wao
wamepoteza raia wawili nao.
Baraza la usalama
la umoja wa mataifa limelaani tukio hilo kwa kauli kali na kuitahadharisha
Kenya kuwa juhudi zozote za kutatua tatizo hilo ni lazima zizingatie haki za
Binadamu.
Kenya imekumbwa na
mashambulizi madogo madogo ya kutumia mabomu ya kurusha kwa mkono tangu
ilipoingiza jeshi lake nchini Somalia kupambana na Al-shabab mwishoni mwa 2011,
ambapo kundi hilo linapigana na serikali ya Somalia kuweza kusimamisha sharia
za kiislaam.
BY: www.habarika.info
BY: www.habarika.info
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako