Sunday 1 September 2013

JUMBA BOVU LAMWANGUKIA DIAMOND PLATNUM



MAMBO yakiwa bado yanaendelea kupamba moto mwendelezo wa Sakata la biashara ya madawa yakulevya “unga” ambalo sasa ni janga kwa taifa letu. Orodha zinaendelea kutoka na kuwekwa wazi huku bunge likivutana kuhusu sakata hlo.
Tetesi za kutoka vyanzo vya ndani zinasema msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul au Diamond ambaye alijitapa wazi mbele ya kamera za habari kuwa anamiliki ukwasi zaidi ya bilioni moja kwenye akaunti yake, nyumba 5 za thamani Kijitonyama na Mikocheni na anatumia simu 6 za thamani ambazo zipo hewani muda wote tayari amenyang'anywa hati yake ya kusafiria na baadhi ya simu zake katika mwendelezo wa uchunguzi juu yake unaofanywa na vyombo vya dola. 
     
Vile vile msanii wa maigizo vichekesho na nyimbo za injili  Masanja Mkandamizaji ambaye anadaiwa kumiliki mkwanja mrefu na nyumba za thamani kubwa mpaka magari kwa muda mfupi naye tayari ametajwa kuhusika na biashara ya sembe.
PataPicha inaendelea kukuletea habari kuhusiana na sakata hili la biashara haram,tuungane mimi na wewe katika vita hii.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako