Sunday 8 September 2013

DENNIS RODMAN NIMERUDI TOKA KOREA KASKAZINI MIKONO MITUPU


Aliyekuwa Mchezaji Maarufu wa Mpira wa Kikapu Nchini Marekani Dennis Rodman kutoka Timu ya Chicago Bulls amesema ya kuwa amerudi akiwa hajapata alichokifuata nchi ya Korea Kaskazini.
Dennis Rodman hakupata ushirikiano mzuri  kutoka kwa Kim Jong Un jinsi ya kumwachia Mmisionari wa Kimarekani Kenneth Bae aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini
Rodman alishidnwa kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo muda ambao aliwasili Uwanja wa Ndege wa Beijing Jumamosi asubuhi.
“Hiyo sio kazi yangu kujibu hayo maswali”aliwajibu waandishi waliotaka kujua kama amefanikiwa alichokifuata Korea Kaskazini
Rodman aliongeza “muulize Obama kuhusu suala hilo, au jaribu kumuuliza Hillary Clinton, sitaki upuuzi kabisa”
Rodman japo safari yake haikuzungumzia ya kuwa anakwenda kujaribu kumuokoa Bae huko Korea Kaskazini

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako