Wednesday 4 September 2013

UKWELI KUHUSU DAYNA KUIBIWA BEAT YA NYIMBO


Ni baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange.
 
Na producer wa nyimbo hiyo akiwa na Shedy clever wa Burn recods.Team tizniz ikaamua kumtafuta Producer huyo ili kujua ukweli juu ya kitu hiki.
Shedy alisema “Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe,alivyokuja Dayna akaupenda ule mdundo,na mimi sikumnyima akafanya demo lakini hakulipia kabisa.Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio pale,akataka kusikia midumdo nikacheza midundo mbalimbali ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna alifanya demo.
Mimi nikampigia Dayna na kumuelezea kwamba diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali kabisa.Mimi sina cha kusema zaidi ila ukweli upo hivyo.

STORY YA DYNA 
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro.
Akiongea na team tizniz Dayna alisema “Kukweli ni nimekwazika sana  pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA  nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo ilibidi nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba.
 Baada ya muda ya nikamtafuta tena vipi ili tufanye kabisa ile nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri lakini.Lakini nashangaa sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo ameeimba yeye tena harafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile  pia na mashairi yale yale.Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri,kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake.Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo.

Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako