Katika hali ya kushangaza na isiyo
ya kawaida mamba mkubwa mwenye urefu wa futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia
chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani
iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa
8.
Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa
hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa
chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.
Alisema
kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo
hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa
chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa
hoteli hiyo.
Inaelezwa kuwa mamba huyo
aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na
kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia
kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye
kwenye chumba hicho usiku mzima.
Mamba ni wataalam wa kujificha na
ndiyo maana hunusurika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa
nje ya maji,alisema Mr Whittall.
Na huweza kutulia sehemu moja kwa
muda mrefu bila kugundulika na mnyama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu
hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au
kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha
mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwa sababu
kulikuwa na joto.
Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita
wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini
ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako