Friday 13 September 2013

KANYE NA KIM KARDASHIAN WASIMAMIA UJENZI WA MJENGO WAO

 
Jengo wanalojenga Kanye West pamoja na Kim Kardashian lenye thamani ya Dolla za kimarekani Million 11 bado linaendelea kuongezewa naksi naksi kwa miezi kadhaa sasa.
Alhamisi wiki hii wapenzi hao walikuwa wakiwalazimisha wajenzi kukamilisha haraka na kwa kiwango cha juu mjengo wao huo wa thamani
 
K & K hao walikuwa wakizunguka zunguka katika eneo hilo lenye ukubwa wa futi za mraba 10,000 wakitathmini mazingira ya mjengo wao, wakiangalia eneo la kufanyia mazoezi (Gym) Saluni ya Nywele, Viyoyozi (Ac’s)
“Tunaimani nyumba yetu itakamilika mapema na kwa ubora tunaoutaka” Alisema Kanye West

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako