BAADA ya mashabiki na uongozi wa
klabu ya Manchester United kuchomwa na mkuki wa moyo kutokana na taarifa za
mshambuliaji wao wa zamani Cristiano Ronaldo kusaini mkataba mpya wa Real Madrid,
nyota huyo amewatonesha jearaha hilo.
Staa huyo wa Ureno aliyekuwa
akihusishwa na madai ya kurudi katika klabu yake ya zamani, jana asubuhi
aliongeza mkataba wa miaka mitatu utakaofikia kikomo 2018 wa kuichezea Madrid
na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Hispania.
Ronaldo hadi sasa ameshaifungia timu
yake ya Madrid mabao 203 tangu alipotua klabuni hapo, amesema hana mpango wa
kurudi tena katika klabu yake ya zamani kwani ile itabaki kuwa historia tu,
sasa yeye ni mchezaji wa Madrid.
"Niwe mkweli kwako. Kila mtu
anajua kuwa nilikuwa Manchester kwa miaka sita, na walinipa vitu vingi na
siwezi kusahau hilo," alisema Ronaldo.
"Lakini Manchester imepita,
sasa ni Madrid. Hana ni nyumbani kwangu, familia yangu ipo hapa. Nina furaha sana
kuwa hapa.
"Ninaiheshimu klabu yoyote
ambayo inagonga hodi na kuniulizia kuhusu mimi, lakini wanatakiwa kujua kuwa
mipango yangu kwa sasa ni kubaki hapa na kuichezea klabu hii labda hadi mwisho
wa maisha yangu ya soka.”
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako