Friday 27 September 2013

KENYA BADO MAMBO SI SHWARI

POLISI wawili wameuawa nchini Kenya wakati watatu wakijeruhiwa baada ya kuvamiwa na kundi linalodaiwa kuwa la Al-Shabab.
Tukio hili limetokea wakati Wakenya wakiwa katika maombolezo ya siku tatu kuwakumbuka watu zaidi ya 60 waliopoteza maisha na 175 kujeruhiwa katika shambulio la Jumamosi iliyopita kwenye jengo la biashara la Westgate.

Shambulio hilo limetokea mapema jana katika kituo cha ulinzi kilichopo karibu na mpaka wa Somalia, mjini Mandera.
Kamanda wa Polisi, Charlton Mureithi ameeleza kuwa mbali na polisi wawili kuuawa na watatu kujeruhiwa kundi hilo limechoma magari 11.

Tukio hili limetokea saa chache baada ya kundi la Al-Shabab kutoa taarifa kuwa mashambulio yataendelea mpaka Kenya watakapoondoa wanajeshi wake nchini Somalia.
Kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Godane Shaykh Mukhtar Abu Zubayr, alitoa onyo kwa Wakenya kuwa hakuna njia yoyote wangeweza "kuhimili vita ya kulipa kisasi ndani ya nchi yao wenyewe" katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao siku ya Jumatano.

"Chagua kuondoa majeshi yenu yote,.." Godane alisema. "Vinginevyo jiandae kwa wingi wa damu itakayomwagika nchini kwenu, anguko la kiuchumi na makazi."

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako