Friday 6 September 2013

PICHA ZA MAMA WA KINIGERIA ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE


    
Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya Dar es salaam jana.
 

Mwanamke  huyo amekamatwa  akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways  na  aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. 
  
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo na   thamani yake,
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako