Klabu
ya Real Madrid imevunja mzizi wa fitina baada ya jana kumalizana na kiungo
mshambuliaji, Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho
iliyovunja rekodi ya pauni 100 milioni.
Mchezaji
huyo raia wa Wales amevunja rekodi ya mchezaji mwenzake wa timu hiyo,
Cristiano Ronaldo a mbaye alisajiliwa kwa ada ya uhamisho ya pauni 80 milioni
mwaka 2009, hivyo kufanya timu hiyo kuwa na wachezaji waliosajiliwa kwa gharama
kubwa.
“Napenda
kuwashukuru kila mtu katika klabu yangu, Mwenyekiti, bodi, wafanyakazi
wote, kocha na wachezaji wenzangu na zaidi mashabiki ambao naamini watanielewa
kwa maamuzi ytangu ya ajabu ya kumaliza maisha yangu katika klabu yangu,"
alisema Bale alipokuwa anazungumza na tovuti ya Tottenham.
“Nina
uhakika kuwa huu ni wakati mzuri kuondoka katika ambayo nilikaa vizuri na
kucheza soka zuri katika siku zote zilizokuwa pale. Najua wachezaji wengi
wanapenda kujiunga na klabu bora yenye wachezaji wenye vipaji, lakini
ninachoweza kusema, ndoto yangu imetimia.
“Pamoja
na kuondoka lakini Tottenham ipo moyoni mwangu wakati wowote na nina uhakika
msimu huu utakuwa wa mafanikio kwao. Sasa naangalia mbele, kinachofuata katika
maisha yangu ni kucheza soka katika klabu ya Real Madrid.”
Wakati Madrid wakikamilisha kumnunua
Bale wamemruhusu kiungo wake, Kaka kutua katika klabu ya AC Milan ya Italia.
Madrid walikubaliana na Milan lakini walikuwa wakisubiri kukamilisha usajili wa
Bale.
STORY BY: MASALU JR
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako