Mwandishi Jamal
Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab
kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate.
Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4
Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4
Jamal
Osman: Kwanini mmefanya shambulio?
Msemaji
wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni
kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea
kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio
walitushambulia na tunajilinda.
Haijalishi
kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe
dhidi ya yule aliyekushambulia.
JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi
mataifa makubwa yatawatafuta?
Msemaji
wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale
wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia
tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya.
Wakenya
wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima
ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama
Wamarekani sababu sisi si wadhaifu.
Na
tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale
wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.
JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?
Msemaji
wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga
mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi
yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao
kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote
tuwezapo.
Sababu
tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi.
Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji.
Ni
sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka
kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.
JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa
tokeo la hili?
Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata
ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa
hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani
Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.
JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu
na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?
Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe
wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu
kama wanataka amani?
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
JO:
Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?
Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo
(Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila
mtu – Kenya ni eneo la vita.
JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana
maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?
Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.
Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya
SOURCE:MUSLIM OF AFRICA
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako