Friday 6 September 2013

VURUGU KUBWA BUNGENI, MBOWE NA MBILINYI WATOLEWA NJE

Baada ya tukio hilo, Ndugai aliwaamuru askari wa bunge kumtoa nje Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ndipo mzozo ulipotokea.

Mheshimiwa Mbilinyi (Mr. Sugu) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge

Hali hiyo ilitokea wakati wa Majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013.
Mbowe aligoma kutolewa nje ya bunge baada ya askari kufika alipokuwa amekaa kwa lengo la kumtoa nje, ndipo ilipotokea sintofahamu na mzozo mkubwa ndani ya bunge hali iliyopelekea wabunge wote wa Chadema kutoka nje.

Wabunge wa Kambi za Upinzani wakitoka Nje ya Ukumbi wa Bunge













Halikama hii pia ilitokea jana wakati muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ukisomwa na kupelekea wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kutoka nje wakishinikiza muswada huo usisomwe hadi maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako