Wednesday 4 September 2013

TYGA ADAIWA KUTOLIPA MADINI ALIYOKOPA

Mwanamuziki anayejulikana kwa jina la Tyga anadaiwa vito vya thamani zaidi ya $ 91,000 alivyokopa kwenye duka la sonara liitwalo Beverly Hills jeweler 
 
Mmiliki wa duka hilo amenukuliwa akimsema Tyga kwa kutembea na vito hivyo vya thamani barabarani huku akiwa hajalipa hela ya kununuliwa madini hayo.
 
Vito hivyo vya thamani ni pamoja na Cheni na Saa zenye thamani ya zaidi ya Milioni 150 alizokopa(kuazima) mwishoni mwa mwaka jana.
 
Mmiliki wa Sonara hiyo Bwana Jason amesema Tyga alitakiwa atoe $ 28,275 August ,2012 kama walivyokubaliana ila hadi sasa hajamalizia hela hiyo na kuendelea kutumia madini hayo.
Jason Beverly amelalamika zaidi na kudai Michael Stevenson (Tyga) aliazima Cheni ya Almasi yenye thamani ya $ 63,000 Desemba 2012 lakini hakuirudisha
Hadi sasa Jason anamdai Tyga gharama hizo pamoja na gharama za kuchelewesha ambazo ni $ 185,306.50 ambazo ni zaidi ya shilling Milion 300.
“Tumemita Tyga na kumpa malalamiko yetu ila hajajibu hadi sasa” Jason alisema
Jason kutoka Beverly Hills Jeweler ndio sonara maarufu inayowavalisha vipuli na madini wasanii maarufu kama Justin Bieber, Mariah Carey, Diddy, Beyonce, naLeBron James. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako