Wednesday, 27 November 2013

UWANJA WA KOMBE LA DUNIA, 2014 WAANGUKA NA KUUA 3


Watu watatu wamethibitika kufariki baada ya uwanja wa Sao Paulo kuanguka.

Akiongea na vyombo vya habari, msemaji wa polisi katika eneo la Sao Paulo amethibitisha vifo hivyo.

Uwanja huo ambao ulitegemewa kufanyika mechi ya uzinduzi wa michuano ya kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Uwanja huo ulitegemewa kuwa umekamilika mwezi ujao, ili uangaliwe na wataalam kutoka FIFA na uweze kuruhusiwa kutumika kwenye michuano inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa Soka duniani.

Uwanja huo ulianza kujengwa Nov. 2012 kwa gharama ya zaidi ya sh. Bilion 400 za kitanzania, mategemeo ya kukamilika Desemba mwaka 2013.

Uwanja wa Sao Paulo ulikuwa unajengwa kukidhi watu 65,000 watakaokaa na kuangalia mechi.

Rais wa FIFA, Sepp Blatter ameandika kwenywe ukurasa wake wa Tweeter "Nimepatwa na majonzi makubwa kupata taarifa za vifo hivyo vya wafanyakazi waliokuwa wanajenga uwanja huo leo natoa salamu za pole kwa wafiwa na familia zao"
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako