Thursday 21 November 2013

BERRY WHITE ACHOMA GARI YA MPENZI WAKE, KISA WIVU.


Mwanamuziki wa kundi liliowahi kuwa pendwa ndani ya Bongo, 2 Berry, Mbaraka Maarufu kama Berry White, amechoma moto gari ya mpenzi wake aitwaye Sayla wanayeishi naye pamoja jijini Dar es Salaam.
Berry white amechoma gari hiyo aina ya Spacio kwa madai ya kusalitiwa na mpenzi wake huyo na hadi sasa bado anashikiliwa na polisi kwenye kituo cha Osyterbay jijini Dar.
Akitoa taarifa hizi kwa Soudy Brown a.k.a Gossip Cop kwenye kipindi chake cha You Heard, baba mzazi wa msanii huyo aliyeko Zanzibar amesema wanafanya kila jitihada wamtoe ndani ya selo kijana wao. 
"Tumepanga kuongea na huyu anayeishi naye tukae kitako kwa upande wangu mimi ntaweza kumfidia tu gari. Wao tunapenda tu wasikilizane na tuko tayari kukaa kitako na mwanamke kumnunulia gari,"amesema mzee huyo
Hata hivyo amekanusha taarifa ya kuwa mwanae amekuwa akifanya matukio mengi ya kihalifu kwa mchumba wake huyo ikiwa ni pamoja na kuuza vitu vyake na kumpiga mara kwa mara.
"Hapana uhalifu mjomba, mimi niko nao hawa ana kwa ana huyu Salya na huyu Mbaraka mwanangu. Ni mambo ya kike kike na ya kiume kiume tu wanafanya matatizo hapa na pale, sio matatizo makubwa kama hayo niliyosikia."
Mzee huyo anayeishi Oman na aliyekuja kwenye msiba wa mwanae mwingine Visiwani Zanzibar, ameongeza kuwa yeye ameshindwa kuja Dar es Salaam kushughulikia suala hilo kutokana na kuwa mgonjwa lakini mkewe, wanae na dada zake pamoja na ndugu wengine wamekuja Dar tayari.
Ameongeza mwanae na mchumba wake wote walikuwepo kwenye msiba wa mwanae mwingine huko Zanzibar na walilala chumba kimoja na hawakuwa na tatizo lolote.
"hivi juzi walikuwa pamoja mazikoni hapa walikuwa wanalala chumba kimoja na mimi, yeye huyo mke na mwanaume mtoto wangu, mimi nimelala juu ya kitanda wao magodoro chini wamelala."
Alimalizia kwa kusema kuwa pindi mambo hayo yakiisha, yupo tayari kuwaozesha wawili hao waishi kihalali kama mke na mume.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako