Monday, 4 November 2013

MHE ZITTO ATOA MSIMAMO WAKE KWENYE SUALA ZIMA LA KUCHUKUA POSHO



Mhe Zitto katika uwanja wake wa Facebook!!.

Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.

Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.

Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk. 

Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako