Wednesday 20 November 2013

HUYU NDIYE MUIGIZAJI WA AFRIKA MASHARIKI ALIYEMKUNA MWANAMAMA OPRAH WINFREY MPAKA KUWA GUMZO MAREKANI


Jina la muigizaji wa Kenya, Lupita Nyongo limeendelea kushika kasi Hollywood. Tangu aigize kwenye filamu ‘12 Years A Slave’, jina la ‘black beauty’ huyo mwenye miaka 30 limeendelea kung’ara.
Pamoja na kwamba Oprah Winfrey anaweza kuwa mpinzani wake kwenye tuzo za Oscar kwenye kipengele cha ‘Best Supporting Actress, amesema anamkubali msichana huyo. “Nilikuwa naye kwenye roundtable ya Hollywood Reporter. 
Nilikuwa nimekaa kufanyiwa make-up na mtengeza nywele aliniangalia kwenye kioo na kunong’oneza  ‘Oprah.’ Nilisema ‘What?!’” ilikuwa kama slow motion. Niliinuka. Niligeuka na alikuwepo pale. Mikono yake ilikuwa imefunguka na alinipa kumbato kubwa, akisema ‘You were amazing!’”

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako