Saturday 23 November 2013

VICTORIA NA BECKHAM WACHANGIA NGUO KUWASAIDIA WAHANGA WA KIMBUNGA UFILIPINO


Mwanadada kutoka kundi la Spice girls ambaye pia ni mke wa Msakata kabumbu maarufu duniani, Victoria Beckham ameonyesha kujali wananchi wa Ufilipino baada ya kuamua kuuza baadhi ya nguo zake ili kuweza kuwasaidia.
Mwanadada Posh na David Beckham walionekana wakipakia mabox 20 ya nguo nyingi zikiwa za zamani alizokuwa anazivaa posh wakati yupo kwenye kundi la Spice Girls.
Pia walikuwa wanapakia Viatu, suti pamoja na mabuti kuyapeleka kwenye shirika la misaada la Nchini Uingereza ili wazinadi na kuwasaidia wahanga wa Kimbunga huko Ufilipino.
"Vitu vingine ni vidogo na tunaweza kuwasaidia wenzetu kama kwetu vitakuwa havitumiki" alisema Beckham.
Suti na majaketi ya mastar hao yanauzwa karibu Shilingi 192,000/= za kitanzania, ambazo zitakusanywa kwa pamoja ili kusaidia wahanga hao.
"kama tukifanikiwa kuuza hapa Uingereza itakuwa vizuri ila ikishindikana tunaweza hata kuuza mtandaoni ili tuwasaidie haraka wahanga wa Kimbunga huko Ufilipino" 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako