Tuesday 26 November 2013

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TOKA SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA


Siku kama ya Leo  tarehe 26, Novemba, 2012 majira ya saa 2 usiku ndipo ziliposambaa taarifa za kifo cha muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ Hussein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’.
Ikiwa imetimia mwaka mmoja toka Sharo atutoke, familia inafanya kisomo kwa ajili ya kumkumbuku huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza, Tanga.
Jana tarehe 25 Novemba, 2013 kulikua na mkesha maalum.
Mkesha huu umeambatana na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa madrasa, Miongoni mwa watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea
Exclusive interview aliyofanyiwa na mama mzazi wa Sharo Milionea pamoja Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel, Azam pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
“Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu, kwa kutaka kumsomea dua ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake, Mpaka sasa mtandao wa Airtel peke yake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa jumla ya milion 10, lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba” Mama yake Sharo Milionea.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na mjomba wake, nikamwambia mjomba wake akiuze kwa sababu ya usumbufu maana mi nipo mbali huku, maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo Mudy Suma ambaye ni rafiki wa marehemu kwa hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari, na kweli Mudy Suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa hiyo movie bado ndo sijapata hela, nimeambiwa ni movie moja ambayo amecheza yeye na kitale na mudy suma’ Mama sharo alimalizia

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako