Tuesday 26 November 2013

NAY WA MITEGO AFANYA YAKE KENYA


Nay wa Mitego yupo Nchini Kenya akiwa amekwenda kufanya Video ya Wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “Nakula ujana” Chini ya Director Kevin Bosco JNR (aliyefanya video kadhaa za Camp Mullah).
Katika picha ambayo ameitupia Instagram akiwa na Mkali kutoka pande hizo za 254 Jaguar na kuandika maneno kuhusu picha hiyo.
Tuna Kula Ujana ni wimbo mpya wa Ney Wa Mitego wenye ujumbe tofauti na nyimbo zake mbili za awali kwani hapa kaimba maisha tofauti ya vijana wa mjini na wanavyoishi.
Ney amezungumzia gharama za Video hiyo kuwa ni Zaidi ya Shiling million 7 za kitanzania na atatumia takribani wiki moja kumaliza ku-shoot kichupa hicho, huku akitangaza wimbo huo Nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako