Thursday 21 November 2013

CHRISS BROWN ALIMLETEA VURUGU MAMA YAKE NA KUFUKUZWA REHAB


Habari kutoka chanzo kikuu cha habari ndani ya marekani,TMZ kimeripoti kuwa mwanamuziki Chriss Brown aligombana na Mama yake mzazi kipindi alipokuwa Rehab(eneo la matibabu ya kuthibiti hasira) akipata matibabu.
Chriss Brown alifanikiwa kukaa ndani ya Rehab kwa muda wa siku 13, kupata matibabu hayo ambayo yalionekana kumsaidia ila baada ya mama yake mzazi kufika kumsalimia na kumtaka akae humo ndani kwa muda mrefu zaidi hapo ndipo hasira zake zikarudi upya na kuvunja kioo cha gari ya mama yake
Mahakama imemuamuru Brown a rudi katika Rehab kwa siku 90 (Miezi 3) ili aendelee na matibabu ya tatizo lake la hasira, na baada ya kushauriana na mwanasheria wake Chriss amekubaliana na uamuzi huo.
Hii inakuja ikiwa ni wiki ambayo Chriss Brown ameachia mixtape yake mpya ya "X-Files" yenye jumla ya nyimbo 5 ambayo aliitoa bure kutimiza ahadi aliyowapa mashabiki wake kabla hajaenda Rehab

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako