Tuesday 26 November 2013

RIHHANA AHAMISHIA MOYO WAKE KWA MKAKA HUYU


Mcheza kikapu Handsome Boy Nick Young anayechezea timu ya kikapu ya Los Angels LAKERS inayoshiriki katika ligi ya kikapu Marekani NBA ameandikwa kwenye vichwa vingi vya habari majuu hivi karibuni kuhusiana na mustakhabali wa mahusiano yake na mwanamuziki Iggy Azaela kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kuvunjika chanzo kikidaiwa ni Bi mdada Rihanna a.k.a Bad Gal  kusaka kwa udi na uvumba penzi la mcheza kikapu huyo.
Chanzo kimoja kutoka majuu kinaeleza kwamba kitendo cha mwanadada Rihanna kuonekana akiwa karibu na Nick siku za hivi karibuni na pia kuwepo katika uwanja ambao ulichezewa mchezo uliozikutanisha timu ya Los Angels LAKERS na WARRIORS ambapo LAKERS iliibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 102 – 95 dhidi ya wapinzani wao, katika mchezo huo mwanadada Rihanna alionekana akimkodolea macho takribani muda wote Nick Young huku akiwa anatamka jina lake pindi mchezaji anapokuwa na mpira hali iliyozua maneno mengi kuwa huenda mama huruma Rihanna anataka kujiweka kwa mchezaji kikapu huyo kwa sasa.
Rihanna ambaye anatamba na ngoma ya ‘Something More’ anafahamika kwa kuvunja amri ya sita  na wanamuziki wengi wanaotamba katika gemu ya muziki nchini Marekani huku rapa kama Meek Mill, Asap Rocky, Chriss Brown, Matt Kemp(LA Dodgers), Nick Minaj, Aston Klutcher(Actor) na wengine wengi  wakitajwa kuwahi kuwa katika mahusiano na bi mdada huyo kwa vipindi tofauti.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako