Thursday 21 November 2013

SAMSUNG WAILIPA APPLE FAINI $ BILION 1, ZABEBWA KWA MALORI 30


Sio kituko bali ni ukweli mtupu.
Leo asubuhi malori 30 yaliwasili katika makao makuu ya Apple Company watengenezaji wa vifaa mbalimbali za mawasiliano, yakiwa yamejaa sarafu za cent 5 zenye thamani ya $ bilion 1 ambazo ni faini iliyotakiwa samsung iilipe apple kwa kunakiri baadhi ya Mambo kwenye vifaa vya mawasiliano.
Watu wakiwa wamejaa na kufurika kushuhudia malori hayo wakiwa hawajui linaloendelea, ndipo Tim Cook mkurugenzi wa Apple Company alipokea simu kutoka kwa Mkurugenzi mwenzake wa Samsung akimjulisha ya kuwa hizo ni pesa za faini alizotakiwa kuilipa kampuni ya Apple.
Kwa kuwa hawakuwa na mkataba wowote wa kuonyesha ya kuwa malipo yafanywe kwa mfumo gani ndio Mkurugenzi wa Samsung alipoamua kulipa Faini hiyo kupitia cent 5 hadi zimefika Dola bilioni 1 ambazo zimejaa kwenye malori 30.
Hivi sasa Mkurugenzi na watendaji wa Apple wanajishauri jinsi ya kuzihifadhi pesa hizo na pia jinsi ya kuzitumia maana ni nyingi na zinahitaji eneo kubwa kuzihifadhi.
Pia kuna changamoto ya jinsi ya kuzihesabu ili kuhakiki ya kuwa zimefika kiasi hicho cha faini waliyotakiwa kulipwa maana itawachukua zaidi ya saa kadhaa kuzihesabu na kuzithibitisha.
Mwenyekiti wa Samsung Lee Kun-hee amewaambia waandishi wa habari ya kuwa wameanza wao kutuletea mchezo mchafu wa kutushtaki kwa kuwaibia baadhi ya hatimiliki wanazosema tumeiba kwenye simu na vifaa vyao vya mawasiliano nasi tukaona njia nzuri ni kuendeleza mchezo huo mchafu kwa kuwapa haki yao ya faini ila faini ambayo itawapa usumbufu kuitumia.
"wanaweza kutumia sarafu hizo kununulia viburudisho kwenye mashine za kuuzia soda au maji ambazo zinahitaji sarafu haitakuwa tatizo, sisi tumemaliza kulipa faini yetu kulingana na hukumu ya mahakama" 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako