Friday 22 November 2013

MAPACHA WATATU KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA LEO


 BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’ leo Ijumaa Nov 22 katika ukumbi wa letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma'

Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho yao ya miaka minne tokea bendi yao imeanzishwa. Pembeni yake wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’
Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.
Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na Wivu.
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo ndani ya kiota cha Etasi (zamani Business Park) uliopo Victoria jijini Dar
Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.
Akizungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.
Bendi ya Mapacha watatu ilianzishwa mnamo mwaka 2009, tarehe 15 mwezi 11 (15, Novemba, 2009) ikiwa na waimbaji Waasisi Jose Mara (akitokea Bendi ya FM Academia) na Khalid Chokoraa (akitokea Bendi ya Twanga Pepeta) ambao ndio wamiliki wa bendi hiyo.
Bendi hadi sasa ina miaka minne (4), na imefanikiwa kutoa Albam mbili, ya kwanza JASHO LA MTU (Iliyopata Tuzo kupitia wimbo wa Shika Ushikacho – 2011, pia rapper Khalid Chokoraa alifanikiwa kupata Tuzo ya Rapper Bora wa Mwaka 2011), albam ya pili inaitwa YARABI NAFSI (iliyozinduliwa March, 2013)

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako