Ndugu
wanahabari, Baada ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi wa rehema.
Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni na
mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku
chache zilizopita huko Afrika ya kusini. Ndugu zangu wanahabari, Wengi
mnanifahamu na kuifahamu vema historia yangu katika utendaji kazi na utumishi
wa umma wa Watanzania. Nimekuwa nikiitumikia nchi yangu kwa kipindi kirefu
katika Nyanja na sekta mbali mbali kuanzia Darasani mpaka kwenye siasa. Kwa
msingi huo, mimi Profesa Juma Kapuya, siku zote ninajikuta mwenye wajibu
endelevu wa kuendelea kulitumikia Taifa langu kila siku mpaka kufikia mwisho wa
Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari, Hivi karibuni nikiwa huku jimboni kuendelea na
shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka Tuhuma kadhaa
zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya
chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku. Tuhuma hizo
zisizokuwa na kichwa wala miguu na pia kutokuwa na ukweli wowote, wamekuwa
wakizitoa kwa kumtumia msichana anayedai amefanyiwa vitendo visivyofaa na mimi.
Mimi simfahamu na sijui hizi shutuma zinatokea wapi. Ndugu wanahabari, Kwa
tamko hili ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa sana na uwezo mdogo wa
kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao haitatimia.
Napenda
niwakumbushe ndugu zangu kwamba tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
na wapinzani wangu wameanza kunichafua ili nionekane sifai. Ninapenda kuwaambia
watanzania na wananchi wa jimbo langu kuwa wanatakiwa wazipuuze taarifa hizi
kwa kuwa hazina ukweli wowote na kwamba ni za kutungwa zenye lengo la
kunidharirisha na kuniondolea heshima yangu niliyojijengea kwenye jamii kwa
kipindi kirefu sasa. Waswahili wanasema dawa ya mjinga ni kumpuuza Na hili
linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa na chombo kimoja tu cha habari
kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na baadhi ya wanasiasa wa chama changu
wasiokitakia heri chama chetu, naomba kuwashukuru na kuwapongeza vyombo vingine
vya habari kwa umakini wenu wa kuwa na nauelewa wa kutoandika kitu bila
kukifanyia uchunguzi na kubaini ukweli ulivyo.
Chombo hiki cha habari kiliwahi
kuripoti mwaka jana kuwa kuna mitambo imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe
na kisha kuufanya uonekane umetoka kwenye namba Fulani, kwa kipindi kile
sikuwaelewa, lakini sasa ninawaelewa na nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndio
waliouingiza mtambo huu na sasa wameamua kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza
meseji na kuzihusianisha na mimi. Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.
Ndugu wanahabari, Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii yangu kwa
kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa miongo
kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna hii.
Kwenye hilo ninawaambia ‘’janja yao nimeigundua, na
hawatafanikiwa’’ Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye kuona hilo jambo lina ukweli
alipeleke kwenye vyombo husika ili lishuhulikiwe kwa mujibu wa sheria na sio
kutumia vyombo vya habari kuchafuana. Mwisho ninasisitiza kuwa nitaendelea
kuilinda na kuitetea heshima yangu niliyojijengea kwa jamii kwa muda mrefu sasa
na sitaruhusukuiona ikiharibiwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.
Tuendelee kuijenga nchi yetu, Mungu Ibariki Tanzania
Imetolewa
tarehe 15.11.2013
nami
Prof. Juma A.Kapuya Mbunge – Urambo Magharibi
S.L.P 45
Kaliua Tabora Simu 0784993930
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako