Saturday 2 November 2013

MTOTO WA BECKHAM, BROOKLYN AANZA MAZOEZI MAN UNITED


 
Mtoto wa Mchezaji maarufu Duniani David Beckham Brooklyn mwenye umri wa miaka 14 ameanza kufanya mazoezi kwenye kambi ya vijana ya Manchester United kuangalia uwezekano wa kuajiriwa kama mshambuliaji wa Timu hiyo pendwa hapa Duniani

Brooklyn ana umri sawa na umri aliokuwanao baba yake wakati anajiunga na Timu ya Manchester United miaka hiyo ya nyuma, ambapo Beckham alifanya vizuri muda mfupi baada ya kuingia kwenye kambi ya vijana ya Timu hiyo.
Wakati Brooklyn akifanya mazoezi na kikosi cha vijana ndani ya Manchester United mdogo wake aitwaye Romeo Beckham ametia saini kuanza mazoezi kwenye kikosi cha vijana washika Mtutu wa London – Arsenal tokea September mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako